Friday, August 27, 2010

JIZI LA CHUPI LABAMBWA

Polisi katika jiji la Tokyo nchini Japani imemtia nguvuni jamaa mmoja ambaye ni mtaalam katika shule ya vipofu nchini humo kwa kwa kosa la wizi wa chupi kwa dobi. Jamaa huyo aitwaye Tsuyosh Hiramo mwenye umri wa miaka 43 alikutwa na Polisi akiwa na chupi 150 za wizi.

Kwa mujibu wa gazeti la Nikkan la Japani aliyeibiwa chupi hizo ni mwanamke mwenye umri wa miaka 22. Tokyo ni moja ya majiji makubwa na yenye vituko vingi hapa duniani.

4 comments:

  1. kuiba chupi Kaaazi kwelikweli!!! yaani nimecheka kweli mpaka mbavu zaniuma, kwani umenikumbusha nami niliwahi kuibiwa chupi wakati naishi Matetereka kijijikimoja huko Madaba Songea.

    ReplyDelete
  2. Huwa akiziiba anazivaa au anafanyia biashara. Duuu, manake mimii nilijua huko ni kwa wenye uwezo, hata chupi?

    ReplyDelete
  3. Yasinta haya mambo yapo mie niliwahi kuona kuna mdada mmoja mrembo Ilala Dar akila kichapo kwa kuwaibia wenzake chupi.

    ReplyDelete
  4. Emu - Three huyu jamaa sijui aalikuwa ana nia gani, ila si unajua watu wa mataifa mengine kwa vituko, labda alikuwa anataka kutengeneza maktaba yake ya chupi!!

    ReplyDelete