Thursday, May 12, 2011

KOMANDOO KUVAA VIATU VYA OSAMA


Unajua kwamba  kundi la kigaidi  la Al  Qaeda lina mpango wa kumkabidhi Ilyas Kashmiri ambaye alikuwa ni Komandoo wa jeshi la Pakisatani, kuwa kiongozi mkuu wa kundi hilo kumrithi Osama Bin Laden aliyeuwawa na majeshi ya Marekani hivi karibuni.. Habari za ndani toka FBI nchini Marekani zinaelea kuwa Kashmiri ni gaidi mwenye nguvu kubwa na ushawishi katika matukio ya maangamizi.

Ilyas Kashmiri alikuwa mmojawapo wa makamanda waliopigana vita  kati ya Afghanistani na Urusi mwaka 1980 na inasemekana alipoteza kidole na jicho moja wakati wa vita hivyo.

1 comment:

  1. Kazi Ipo. Hii dunia hii we acha tu. Joka walikata kichwa halafu kingine chaota...

    ReplyDelete