Tuesday, March 30, 2010

MIKUMI NATIONAL PARK

Mikumi ni moja ya hifadhi mashuhuri na kubwa nchini Tanzania. Eneo kuu na muhimu katika hifadhi hii ni uwanda wa mafuriko pamoja na safu za milima ambazo zinapatikana ndani ya hifadhi hii. Mbuga za wazi ndizo zinazoshamiri katika uwanda wa mafuriko na kuishia katika misitu ya miombo inayofunika mabonde yaliyo chini ya hifadhi.
Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa 3230 na ipo umbali wa kilometa 283 magharibi mwa Dar ea Salaam. Aidha hifadhi hii iko kaskazini ya mbuga ya Selouse na iko njiani unapoelekea katika hifadhi ya Udzungwa, Selouse na Ruaha kwa barabara kutoka Dar ea Salaam na Inapatikana katika Mkoa wa Morogoro.
Unajua kwamba watalii wa ndani wameongezeka katika mbuga hii? Idadi ya watalii wa ndani imeongezeka kuliko miaka mitano iliyopita mwaka 2003/4 na mwaka 2008/9 idadi ya watalii wa ndani imeongezeka kutoka 10,358 hadi kufikia 17, 468 ikiwa ni ongezeko la asilimia 69.

No comments:

Post a Comment