Monday, March 29, 2010

MFUMUKO WA BEI WASHUKA

Taasisi ya takwimu ya Taifa nchini Tanzania (NBS), imesema mfumuko wa bei nchini umepungua kwa asilimia 9.6 kwa mwezi uliopita wa February.
Hiyo ilikuwa mara ya kwanza tangu Agost 2008, na serikali ina uhakika kwamba mfumuko huo utaendelea kupungua katika miezi michache ijayo. Pamoja na hayo baadhi ya wachumi wana mashaka kama malengo hayo yatafikiwa kutokana na uvunaji mdogo wa mazao ya kilimo.
Mchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Geoffrey Mwambe akizungumzia takwimu hizo anasema ana matumaini kwa hali ilivyo uchumi wa nchi unaendelea kuimarika.

No comments:

Post a Comment