Saturday, March 27, 2010

UKEKETAJI UNAENDELEA KILINDI

Wanawake wa jamii ya Kimasai wilayani Kilindi mkoani Tanga wameeleza wazi wazi kuwa wimbi la ukeketaji bado linaendelea japo kwa usiri mkubwa na wakati mungine usababisha vifo. Wakina mama hao walisema pamoja na kufanya jambo hilo kwa usiri mkubwa pia wamekuwa wakiuguza mabinti zao majumbani wakipata majeraha sehemu za siri baada ya kukeketwa na wakati mungine kupoteza maisha. Kina mama hao walifika mbali pale walipo sema walidhani hakuna mwanamke ambaye hajakeketwa duniani.

No comments:

Post a Comment