Thursday, March 25, 2010

UMESIKIA HII?

Mwanaume mmoja mzinzi nchini Marekani ambaye alikuwa na tabia ya kumlawiti farasi wa jirani yake amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu. Jamaa huyo aitwaye Rodell Vereen wa South Carolina nchini Marekani amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu baada ya kukamatwa live akimwingilia farasi kinyume cha maumbile yake.
Vereen alionekana live akifanya kitendo hicho katika video za kamera za ulinzi zilizotegeshwa na mmiliki wa farasi hiyo baada ya farasi wake mwenye umri wa miaka 21 kuanza kuonyesha tabia za ajabu ajabu.
Mmiliki wa farasi huyo, bibi Barbara Kenley, alisema kwamba alianza kushuku kuna kitu kinaendelea baada ya farasi wake kuanza kuonyesha tabia zisizoeleweka na kuanza kupata maambukizi ya magonjwa mbalimbali. Je unajua hii?

No comments:

Post a Comment