Tuesday, April 27, 2010

IJUE MOTOKAA

MotokaaNAJUA WAJUA (jina limetokana na neno la Kiingereza "motor car", mara nyingi huitwa  gari) ni chombo cha usafiri kinachotembea kwenye nchi kavu kikitumia nguvu ya injini au mota yake.
Kuna aina nyingi za motokaa; magari madogo hubeba abiria tu na gari dogo la kawaida hubeba dereva pamoja na abiria hadi wanne. Magari makubwa kidogo hubeba hadi watu 8.
Mengine ya kubeba abiria ni mabasi ambayo ni pia aina ya motokaa lakini mara nyingi hutajwa kama kundi la pekee, sawa na malori ambayo ni motokaa kubwa za kubeba mizigo. Kuna aina tofauti/nyingi za motokaa.

Motokaa huwa na injini (mota) inayosukuma magurudumu kupitia giaboksi. Injini pamoja na magurudumu na bodi hushikwa na fremu ya gari (Chesesi). Magari madogo ya kisasa huwa na bodi inayojibeba yenyewe bila fremu ya pekee. Motokaa nyingi huwa na magurudumu manne lakini magari mazito sana kama lori au basi mara nyingi huwa na magurudumu ya ziada.
 Najua wajua nakukumbusha tu!

No comments:

Post a Comment