Friday, April 16, 2010

KIFARU CHA KIJESHI

Kifaru ni mashine ya vita iliyopewa jina lake kutokana na mnyama wa pori. Kimsingi kifaru ni kama gari kubwa lililokingwa kwa mabamba ya feleji likibeba silaha mara nyingi mzinga.
Vifaru vyepesi hutembea kwa matairi lakini vifaru vizito huwa na minyororo. Mashine ndogo na nyepesi yenye kasi kubwa hupewa jukumu la kupeleleza uwanja wa vita na hasa kubeba askari wakielekea penye hatari.
Mashine kubwa na nzito yenye bunduki kubwa mara nyingi hutumiwa dhidi ya vifaru vya adui. Vikiwa na mbio vinaweza kupita hata moto wa mizinga.
Vifaru vingine hupewa kazi kama lori yaani kubeba mizigo ya pekee kwa kazi inayotekelezwa katikati ya mapigano. Mfano wake ni kifaru kinachobeba daraja la kuwekea juu ya mito midogo. Vingine hubeba roketi dhidi ya ndege au kuhudumia kama mashina ya radar.

No comments:

Post a Comment