Friday, August 6, 2010

AINGIA KATIKA REKODI ZA DUNIA KWA KUKAMATA MBU WENGI

Mwanamke mmoja nchini Taiwan ameingia katika rekodi ya dunia ya kukamata mbu wengi katika shindano lililofanyika nchini humo. Mwanamama huyo aitwaye Haung Yu-yen aliwashinda wenzake 72 kwa kukamata mbu wapatao milioni nne nakujishindia zawadi ya dola za kimarekani 3000.
Shindano hilo liliandaliwa na kampuni ya kutengeneza mitego ya kuuwa wadudu iitwayo Imbicts International. 

Shindano hilo ni moja ya kampeni za kutokomeza mazalia ya mbu ambao wanaeneza ugonjwa wa dengue fever.

No comments:

Post a Comment