Thursday, August 5, 2010

MAMA ATUPA MTOTO CHOONI

Umesikia hii ya mkazi wa Mabibo jijini Dar es salaam aitwaye Helena Silvester mwenye umri wa miaka 34 amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na shitaka la kumtupa chooni mtoto wa kumzaa mwenyewe. Inasemekana alitenda kosa hilo siku ya tarehe 27 Julai 2010 huko mabibo Luhanga majira saa nane mchana saa moja toka kujifungua. Mshitakiwa alikana shitaka na yupo rumande kwa kukosa wadhamini. Hakimu Sundi Fimbo ameahirisha kesi hiyo hadi Agost 18 mwaka huu.

2 comments:

  1. Jamani inakkuwaje, hivi kama yeye angetupwa angekuwepo hadi leo, anahitaji uhakiki wa akili yake

    ReplyDelete
  2. Hizi ndio siku za mwisho mambo mengi ya ajabu yanatokea.

    ReplyDelete