Tuesday, August 10, 2010

ONGEZEKO LA MBU HOSPITAL MUHIMBILI

Hivi karibuni kulitoke ongezeko la mbu ambalo halijawahi kutokea katika historia ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Ongezeko hilo lilisababisha Taasisi ya taifa ya kupambana na malaria (MNCP) kufanya uchunguzi wa kina na kugundua kwamba mbu hao hawana uwezo wa kusambaza ugonjwa wa malaria. Mbu hao wa aina ya Culex ambao upatikana kwa wingi ukanda wa pwani hawana uwezo wa kusambaza malaria, mbu mwenye uwezo wa kusambasa ugonjwa wa malaria ni aina ya Anopheles.
Hata hivyo taarifa za kitaalam zinasema mbu aina ya Culex ni mbu walio katika kundi la mbu sumbufu na ueneza ugonjwa wa babusha na matende.

No comments:

Post a Comment