Thursday, August 12, 2010

MTOTO AUWAWA KIKATILI NA MZAZI WAKE

Mtoto mwenye umri wa miaka 14 aitwaye Frank Ganyala ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Pius Msekwa wilayani Ukerewe mkoani Mwanza ameuwawa kikatili baada ya kuchomwa kisu na baba yake mzazi wakati akiamulia ugomvi wa wazazi wake. Tukio hilo lilitokea nyumbani kwao katika kijiji cha Bungombe.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza Simon Sirro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema baba huyo alichukua uamuzi huo wa kikatili baada ya kuchukizwa na kitendo cha mtoto huyo kuingilia kati ungomvi kati yake na mkewe, mtuhumiwa ameshafikishwa Mahakamani kwa kutenda unyama huo.

2 comments:

  1. Ni kweli huo ni unyama wa kikatili kabisa. Mara nyingi inasemwa kuwa kama wazazi wanagomban wasigombane mbele za watoto. Natumai atapata adhabu.

    ReplyDelete
  2. Ni imani yetu hatua za kisheria zitachukua mkondo wake.

    ReplyDelete