Thursday, August 19, 2010

PENYE MAFANIKIO YA MWANAUME BASI NYUMA KUNA MWANAMKE

Kumekuwepo na msemo/imani kwamba mwanaume yeyote aliyefanikiwa duniani nyuma yake kuna mwanamke. Hii inaaminika kuwa mtu akiwa na familia bora yenye amani na upendo kati ya mume na mke basi ni lazima watafanikiwa.

Na mara zote watu (wanaume) wenye umaarufu ama wenye nafasi nyeti na muhimu katika jamii wanapofanikiwa kwa jambo lolote sifa zinaenda kwa mwanamke (mkewe) pia. Kwa hilo tunawapongeza mama zetu (wanawake) kwa kuwa ni chachu ya mafanikio ya mwanaume. Kwani penye mafanikio ya mwanaume nyuma yake kuna mwanamke.

Je! mwanaume anapokosa mafanikio katika hali yoyote ile na nyuma yake kuna mwanamke, huyo mwanamke atakuwa amechangia kukosekana kwa mafanikio ya mwanaume? Na huyo mwanamke tutamuweka katika kundi gani kwa kutochangia mafanikio ya mwanaume?

Wadau naomba mawazo/majibu yenu juu ya hili.

2 comments:

  1. Kama tunataka usawa kutokana na huo usemi inabidi tukubali yote, kama kuna mafanikio ya mwanaume nyuma kuna mwanamke na kama kuna kutokuwa na mafanikio halikadhalika nyuma yupo mwanamke, kama watu hawa wanaishi pamoja! Huo ni usemi wa kijumla(nadharia), lakini sio lazima kwa wote

    ReplyDelete
  2. Mie naona kuna haja na kina baba kubadilimka kudai haki zao maana kila jambo mwanamke, si wanataka usawa bwana kwa hili mwanaume asipofanikiwa tumkee mkewe!

    ReplyDelete