Tuesday, September 7, 2010

NINO HERNANDEZ MTU MFUPI ZAIDI DUNIANI

Edward Nino Hernandez maarufu kwa Nino mwenye umri wa miaka 24 raia wa Colombia, amefanikiwa kuishika rekodi ya kuwa mtu mfupi kabisa duniani, baada ya kuwekwa katika orodha ya kitabu cha Guinness World Records.

Jamaa huyo mwenye urefu wa inchi 25 (sentimeta 70) na uzito wa kilogram 10 (22Ib) anasumbulia wa ugonjwa wa macho, tatizo lililosababisha kupungua uwezo wake wa kuona na anatarajiwa kuwafanyiwa upasuaji kutoa mtoto wa jicho.

Nino anatoka mji wenye wakazi wengi masikini sana nchini Colombia wa Bogota, na alisema anafurahia ufupi wake kwa unamfanya awe mtu wa kipekee ila hapendezewi na kitendo cha watu kumshangaa, kumshika na wakati mungine kumbeba. Nino ana rafiki wa kike aitwaye Fanny mwenye umri wa miaka 18 na urefu wa futi 5.

No comments:

Post a Comment