Monday, September 6, 2010

WIZI WA DAWA NI TATIZO AFRIKA

Tafiti zimethibitisha kuwa dawa za kutibu ugonjwa hatari wa maralia huibwa mara zitolewapo barani Afrika kwa ajili ya kutibu watu waliopata maradhi hayo. Dawa hizo ambazo utolewa katika serikali za nchi za kiafrika ufikia mikononi mwa wajanja wachache baada ya kufika barani Afrika.

Ripoti iliyochapichwa na jarida moja la matibabu ilibainisha kwamba katika miji kumi na moja barani Afrika kuligundulika kuwa moja kati ya ishirini ya dawa ilikuwa mali ya Zahanati na Hospitali za serikali. Wataalam wengine wamethibitisha kuwa matokeo hayo ya utafiti ni ya kweli na ugonjwa huo upoteza maisha ya watu zaidi ya milioni moja kwa mwaka barani Afrika pekee.

No comments:

Post a Comment