Thursday, March 31, 2011

HESHIMA KWA MWANAMKE

Acheni niwape heshima iliyotukuka wanawake woote;
IMAGINE:
ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa anakusamehe halafu anasahau!!!
UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anakuchukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni kuchukiwa atachukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!
UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI: Anakukaribisha, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.
UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!
CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza tokea hii; hana kinyongo!
UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruwale imenyooshwa kama ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana kashasahau na kukusamehe!
UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!
Na mengine meeeeengi sana wanafanyiwa hawa watu lakini WANASAMEHE, WANAVUMILIA! Ni watu muhimu sana hawa watu maishani mwangu!
HIVI INGEKEWA WANAUME

TUNAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?

Kwa leo acheni tu niwape

heshima zao wanawake wote:
I SALUTE AND LOVE THEM WOMEN!

2 comments:

  1. Wanaume wana moyo mdogo sana, hawawezi. Ye hata kama analala nje anaona poa tu, ila mke akilala nje inakuwa ishu! Kweli mkuki kwa nguruwe......!

    ReplyDelete
  2. Asante sana kwakutambua mchango wetu!!!pamoja na yote hayo huyo mwanamke kiundani hana mapenzi tena,analea watoto na kuishi kwa mazoea tuu,utakuta baadhi ya wanawake wenye kufanyiwa visa hivyo,hasa wazamani anasema nitaenda wapi na wanangu je?.

    ReplyDelete