Wednesday, April 6, 2011

MWANAMKE NA YANAYOMSIBU

Wakati dunia hivi karibuni imetoka kusheherekea siku ya mwanamke katika dunia yetu ikiwa ni pamoja na kukumbushana haki za msingi za mwanamke wa dunia ya sasa, bado mwanamke anaendelea kupata kipigo toka kwa mwanaume na kuonekana kama ni haki yake ya msingi. Tuungane kutokomeza unyama huu kwa mama na dada zetu kote ulimwenguni.

3 comments:

  1. Jamani amemkosea nini kikubwa cha kumpatia kipigo hiki?.Hivi kwani kupiga ndiyo dawa?Hivi kwa maumivu haya kuna mapenzi kweli?Utu ukowapi hapa?jamani dawa ni kukaa chini kumaliza matatizo yenu si kuumizana hivi!! kweli mtoto wa mwenzio unamuumiza kiasi hiki kuna Amani,upendo,utuwema,huruma na kusameheana?

    Aggghhh sijui nani atanipatia jibu!!!!

    samahani @kaka Seif nimewaza kwa sauti!!.

    Pole mwanakwetu!!.

    ReplyDelete
  2. Yaani hili swala sijui litaisha lini? Mara nyingi nimekuwa nikijiuliza hivi pale mtu ampigapo mwenzake anapata nini? na je asipompiga anapungukiwa nini? Hakika inaumiza sana kuona hili bado lipo ....:-(

    ReplyDelete
  3. OMG! I dont believe what im seeing, ni kweli hiyo au ni photoshop, Duh kweli kuna binadamu hawana huruma, mwili umenisisimuka kweli wanawake wanateseka!

    ReplyDelete