Friday, March 12, 2010

BAGAMOYO MJI MKUU WA KOLONI LA KIJERUMANI

Najua hii wajua ila nakukumbusha kuwa mnamo Aprili 1888 Sultani wa Zanzibar alikodisha eneo la pwani kwa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki walioanzisha makao makuu yao Bagamoyo. Ukali wa kampuni ulisababisha katika muda wa wiki chache ghasia ya wenyeji wa pwani kuanzisha vita ya Abushiri na kuangamizwa na wanajeshi wa Ujerumani. Mwaka 1890 serikali ya Ujerumani ilichukua madaraka ya utawala badala ya kampuni, halafu mji mkuu ukahamishwa Dar es Salaam.

Umuhimu wa Bagamoyo ilianza kupungua tena kwa sababu meli kubwa zilitumia bandari ya Dar es salaam badala ya Bagamoyo.

No comments:

Post a Comment