Friday, March 12, 2010

BAGAMOYO NA HISTORIA YA KALE


Je wajua hii? Bagamoyo iko kati ya miji ya kale kabisa ya Waswahili katika Tanzania. Maghofu ya Kaole (msikiti na makaburi ya karne ya 13 BK) yako karibu na Bagamoyo yakionyesha umuhimu wa utamaduni wa Kiislamu katika eneo hili. Lakini hakuna uhakika kuhusu historia ya Bagamoyo ya kale isipikuwa ya kwamba mnamo karne ya 18 mji haukuwa muhimu. Wakazi walio wengi wakati ule walikuwa wavuwi na wakulima, palikuwa na biashara kiasi cha samaki na chumvi.

No comments:

Post a Comment