Friday, March 12, 2010

MJUE SAMAKI NA JAMII YAKE


Samaki ni wanyama wenye damu baridi wanaoshi kwenye maji ya mito, mabwawa, maziwa au bahari. Wote ni vertebrata yaani huwa na uti wa mgongo. Wanatumia oksijeni iliyopo ndani ya maji kwa kuvuta maji kwenye mashavu yao. Kuna aina nyingi za samaki wadogo wenye urefu wa sentimita moja na wakubwa wenye urefu hadi mita 15. Ila tu viumbe vikubwa kwenye maji si samaki bali nyangumi ambao ni mamalia.

No comments:

Post a Comment