Friday, April 2, 2010

SIKU KUU YA PASAKA

Pasaka ni jina la siku kuu muhimu katika dini ya Uyahudi na Ukristo. Jina la pasaka limetokana na neno la kiebrania "Pasakh". Pasaka ya Kiyahudi ni siku ya kumbukumbu kwa Wanawaisrael kutoka Misri wakati wa mwaka 1200KK.

Pasaka ya Kikristo ni siku kuu ya kukumbuka kufufuka kwa Yesu Kristo, mtu ambaye wakristo wanamchukulia kuwa ni mkombozi wao. Yesu alifufuka ikiwa siku ya tatu baada ya kusulubiwa na kufa. Inahesabiwa kuwa ni siku kuu muhimu kabisa katika Ukristo.

Najua wajua ila nakukumbusha tu, ila kwa asiyejua nakuelimusha, hii ndio "PASAKA"

                        "PASAKA NJEMA"

No comments:

Post a Comment