Sunday, May 23, 2010

IJUE FESTULA

Festula ni tatizo linalotokana na jeraha wanalolipata kina mama wakati wa kujifungua baada ya kupata uchungu kwa muda mrefu na pia kuwa na njia ndogo ya uzazi kiasi kwamba kichwa cha mtoto kinashindwa kupita kwa usalama wakati wa kujifungua.
Mgandamizo huo wa mtoto usababisha tundu katika njia ya uzazi na kibofu cha mkojo na mara njingine katika njia ya haja kubwa na kusababisha mwathirika kutoka na haja bila mpangilio au kujizuia. Kutoka huko na haja hovyo, wengi wenye tatizo hili ulazimika kuishi kwa hali ya aibu na mara nyingine hutengwa na wanaume zao na jamii inayowazunguruka.
Kwa mujibu wa shirika la Afaya duniani (WHO) takribani wanawake milioni nne ulimwenguni kote wanaishi na festula na wengine 50,000 hadi 100,000 wanapata tatizo hilo kila mwaka. wengi wao wanaishi Afrika na Asia ya Kusini.

No comments:

Post a Comment