Thursday, May 20, 2010

MAOMBI 23,000 VYUO VIKUU YAFANYIWA KAZI

Tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) imesema katika  kipindi cha mwezi mmoja, tangu wanafunzi waanze kuomba kujiunga vyuo mbali mbali hapa nchini kwa njia mpya ya mtandao, tayari zaidi ya maombi 23,000 yamefanyiwa kazi. Wanafunzi hao walioomba kujiunga na elimu ya juu nchini ni kati ya 60,000 hadi 70,000 ambayo TCU imejiwekea malengo kuwafanyia udahili. Wanafunzi wanaoruhusiwa kutumia mfumo huo ni wale waliomaliza kidato cha sita kati ya mwaka 1988 hadi 2010. Wanafunzi waliochaguliwa na wasiochaguliwa hupewa taarifa kwa barua pepe ama ujumbe mfupi (sms).

No comments:

Post a Comment