Wednesday, May 12, 2010

IJUE KOMPYUTA (COMPUTER)

Tarakilishi (kompyuta) ni mashine inayotumia data kwa njia tofauti kutokana na maagizo zilizoandikwa kwenye bidhaa pepe (kwa Kiingereza software).
Maneno Kompyuta na Ngamizi yanaweza kutumika badala Tarakishi.
Teknolojia hii ni mabadiliko ya kisayansi yaliyowekwa kwenye nadharia ya utendaji kazi. Mabadiliko hayo yanapochochewa kwa kiasi kikubwa huwezesha mambo mbalimbali kuvumbuliwa na kuweza kuboresha shughuli mbalimbali za kijamii, kiuchumi na hata mawasiliano.
Kompyuta ni moja kati ya nyenzo zilizotokana na mabadiliko ya teknolojia ya hali ya juu.
kompyuta inafanya kazi kwa wepesi wa hali ya juu kiasi kwamba unaweza kutafuta kitu kwa muda wa sekunde chache tu, kitu ambacho kama utakitafuta kupitia chombo chengine unaweza kuchukuwa wakati mrefu mpaka kukipata na pengine usikipate, kwa mfano unaweza kufanya hesabu ngumu kwa muda mchache kuliko kutumia akili yako. Pia unaweza kutafuta somo lolote kupitia internet kwa kutumia muda mfupi kulipata somo hilo kuliko ungetumia marejeo ya vitabu vya kuchapishwa.

No comments:

Post a Comment