Tuesday, May 25, 2010

LIJUE BUNGE LA TANZANIA

Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ni chombo cha kutunga sheria na pia ni moja ya mihimili mitatu ya dola. Mihimili mingine ni serikali na mahakama. Bunge la Tanzania linafata mfumo wa " Westminster " uliorithiwa kwa wakoloni wa kiingereza waliowahi kuitawala Tanzania kama wakoloni hapo zamani, katika nchi zinazofuata mfumo huu, waziri mkuu ndiye kiongozi mkuu wa serikali bungeni.
Shughuli za bunge usimamiwa na mbunge aliyechaguliwa kuwa kiongozi wake, kwa Tanzania kiongozi huyo anaitwa spika wa bunge.
Mbali na kutunga sheria bunge linajukumu la kufatilia na kusimamia utendaji wa serikali. Ni kwa sababu hii mara kwa mara unaona wabunge wakikosoa utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji wa serikali.

No comments:

Post a Comment