Saturday, May 29, 2010

LIFAHAMU ZULIA (KAPETI)

Ufumaji wa zulia (kapeti) ulianza karne kadhaa kabla ya Kristo, ilipofika karne tano kabla ya Kristo utengenezaji wa kazulia ulifikia kiwango cha juu cha stadi hiyo ya ufumi. Hayo yalithibitishwa na mgunduzi wa mambo ya kale wa Kirusi, profesa Rudenko ambaye mwaka 1949 aligundua zulia lililo la kale zaidi duniani  katika bonde la Pazyryk, kadri ya futi 5000 katika milima ya Altai huko Siberia. Zulia hilo lilikutwa katika kaburi mithili ya handaki (la mtawa Cyrus) lilikadiliwa kuwa la miaka 2400 mpaka 2500 iliyopita. Historia ilithibitisha kwamba Uajemi (Persia) imebaki kuwa sehemu kuu ya ustadi wa ufumi na ushonaji mazulia duniani. Malighafi ya kufumia mazulia ya kiajemi ni manyoya ya kondoo na mbuzi. Kutokana na muingiliano wa mila na desturi kwa miaka ya hivi karibuni stadi ya ufumi wa mazulia imeenea  duniani na ubunifu umekuwa mkubwa zaidi. Na sasa watu hutumia plastiki, vitambaa, nyuzi za katani n.k. katika kuboresha uzuri na ubora wa mazulia.

No comments:

Post a Comment