Sunday, May 2, 2010

MLIMA KILIMANJARO

Kilimanjaro ni mlima mrefu kuliko yote Afrika. Mlima huu uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro. Una urefu wa futi 19,340 (mita 5,895). Hali halisi ya mlima wa Kilimanjaro ni zaidi kuliko mlima kwani una safu ndogo za milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira.
Kilimanjaro ni wenye asili ya volkeno iliyolala kwa sasa. Kwenye kilele cha Kibo bado kuna gesi inayotoka. Kumbukumbu za wenyeji zinasema kulitokea mlipuko mnamo mwaka 1730.
Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru Peak. Mtu wa kwanza wa kufika kileleni hapo alikuwa anaitwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller tarehe 6 Oktoba, 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani. Wakati ule waliita ncha ya juu "Kaiser-Wilhelm-Spitze" (kijer.:Kilele cha Kaisari Wilhelm) kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani.

No comments:

Post a Comment