Wednesday, May 5, 2010

TELEVISHENI ZANZIBAR NA HISTORIA YA BARA LA AFRIKA

Kituo cha Televisheni cha serikali ya mapinduzi Zanzibar (TVZ), ndio kituo cha kwanza cha televisheni kusini mwa jangwa la Sahara kurusha matangazo yake kwa rangi. Kituo hiki kilianza kurusha matangazo yake mwaka 1973 kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza na matangazo yake kupatikana katika maeneo ya Unguja, Pemba, Dar es salaam,Pwani na Mombasa nchini Kenya. Kituo hicho kikongwe kinabaki katika historia ya bara la Afrika kwa kuwa ni moja ya vituo vya kwanza kabisa. Ujezi wa kituo hiki pichani hapo juu ni wazo la rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Abeid Aman Karume. Jengo hilo la studio maarufu kwa jina la KARUME HOUSE.

No comments:

Post a Comment