Friday, June 25, 2010

IJUE MELI

Meli ni chombo kikubwa cha usafiri kwenye maji. Siku hizi meli huwa na bodi ya chuma ikisogezwa kwa nguvu ya injini inayochoma diseli. Hadi karne ya 19 meli zilijengwa kwa kutumia ubao zikasongezwa hasa kwa nguvu ya upepo kwa kutumia tanga. Jahazi ziko hadi leo.
Meli hutumiwa hasa kwa kubeba mizigo na abiria. Kuna pia meli za kijeshi zinazoitwa manowari.
Kuna njia mbalimbali kutofautisha ukubwa wa meli na njia ya kawaida imekuwa tani GT inayotaja mjao wa chombo.
Mkuu na kiongozi kwenye meli anaitwa nahodha. Watu wanaofanya kazi kwenye meli kwa jumla ni mabaharia.
Mnamo mwaka 4000 KK watu wa Misri ya Kale walimeanza kutengeneza jahazi ndogo. Manmo 1200 KK watu wa Finisia na Ugiriki ya Kale walijenga jahazi kubwa zaidi yenye urefu wa mita 30. Wachina naowalijenga jahazi kuanzia 2000 KK. Waroma wa Kale walitengeneza meli iliyobeba watu 1,000. Katika mazingira ya Mediteranea meli hizi za kwanza zilisogezwa kwa kasia pamoja na tanga. Meli kubwa za kiroma zilikuwa na kasia kubwa zilizopigwa na watumwa wawili au watatu kwa kila kasia.
Jahazi ziliboreshwa hadi kuvuka bahari kuanzia karne ya 15 BK. Wachina na Wareno ni watu wa kwanza waliovuka bahari za mbali. Ila tu Wachina baada ya kutembelea mara kadhaa pwani za Afrika chini ya Zheng He mnamo mwaka 1400 waliamua kuacha upelelezi huu lakini Wareno waliendelea kuvuka Afrika na dunia yote na kuanzisha kipindi cha ukoloni cha Ulaya.
Katika karne ya 19 injini ya mvuke ilipatikana hata kwa meli. Meli zikawa kubwa zikaendelea kukua wakati injini ya diseli imepatikana katika karne ya 20.

No comments:

Post a Comment