Wednesday, June 30, 2010

UNAJUA KWAMBA WATU WAFUPI WAPO HATARINI ZAIDI KUPATA MARADHI YA MOYO?

Jarida la European Heart Journel limewasilisha utafiti uliofanywa kwa muda wa miaka hamsini (50) na kushirikisha watu wapatao milioni 3, inasemekana mtu mfupi yupo katika hatari zaidi ya kuugua na kufa kwa maradhi ya moyo kuliko mtu mrefu kwa asiliamia 50. Utafiti huo uliongozwa na Dr Tuula Paajen wa chuo kikuu cha Tampare nchini Finland, Daktari huyo alisema pamoja na unene, uzee na kiasi kikubwa cha kolestro mwilini kuwa ndio chanzo kikubwa cha kupata magonjwa ya moyo, ufupi nao ni tatizo kwa ugonjwa huo. Kutokana na watu wafupi kuwa na mishipa midogo ya damu Coronary Artery.

No comments:

Post a Comment