Friday, July 2, 2010

JE WAJUA UMUHIMU WA BAHARI?


Bahari ni eneo kubwa penye maji ya chumvi. Katika Kiswahili cha kila siku neno hili hutumiwa pia kwa kutaja magimba madogo zaidi ya maji kama ziwa.
Kwa maana ya kijiografia bahari hasa ni bahari kuu ya dunia yaani maeneo makubwa ya maji ya chumvi ambayo ni kama gimba moja. Bahari kuu ya dunia inafunika asilimia 71 za uso wa dunia.
Tena neno "bahari" linatumika pia kwa maeneo ambayo ni bahari za pembeni za bahari tatu kubwa kama vile Mediteranea, Baltiki.
Bahari ni muhimu sana kwa ajili ya maisha na hali ya hewa duniani. Bahari zinashika asilimia 96.5 za maji yote ya dunia. Maji ya bahari yana takriban asilimia 3.5 za chumvi ndani yake. Kiwango hiki hutofautiana kidogo katika sehemu mbalimbali kutokana na uvukuzaji mkubwa penye joto kwa matumizi ya kibindadamu hata kwa matumizi ya mimea na wanyama wa nchi kavu haifai. Lakini bahari pia ni chanzo cha mvua kwa sababu mawingu hutokea hasa juu ya bahari. Katika mwendo wa uvukizaji chumvi inabaki na mvuke unapaa bila chumvi ndani yake kuwa mawingu na kurudi katika mwendo wa usimbishaji. Usimbishaji unaleta maji yanayojaza mito na maziwa hata akiba za maji chini ya ardhi.
Tangu zamani bahari ni njia kuu za mawasiliano ya kimataifa. Hadi leo asilimia 92 ya mizigo yote hubebwa kwa meli baharini kati ya bandari

2 comments:

  1. ahsante mkuu hapa nimeelimika kuhusu bahari. Hiki ni kiswahili je ukija kwenye kiingereza ipi ni ocean na ipi ni sea? Maneno haya huwachanganya wengi na mimi nikiwemo.

    ReplyDelete
  2. Mkuu ngoja tulifanyie kazi, ahsante sana!

    ReplyDelete