JAMANI! TUWE TUNASOMA UJUMBE MARA TUUPATAPO!!! Mgonjwa mmoja mahututi alikuwa hawezi kuongea, alipofikishwa hospitalini akawekewa oxgen. Bac mchungaji akaja kumuombea. WAKATI AKIOMBEWA, yule mgonjwa akachukua kalamu na karatasi, Akaandika haraka haraka na akampa yule Mchungaji. Ambaye badala ya kuisoma ile karatasi, akaitia kwenye mfuko wa joho na kuendelea na maombi hadi yule mgonjwa, AKAKATA ROHO. Mchungaji hakuisoma ile karatasi akijua kua ni wosia wa marehemu. Akasubiri baada ya mazishi kwenye kikao cha ndugu akasema; "KUNA KITU NILIPEWA NA MAREHEMU SIKU NILIYOKUA NAMUOMBEA" Akampa mmoja wa wanandugu akisome. Haya ndiyo yaliyokuwa yameandikwa na yule mgonjwa: "UMEKANYAGA WAYA WA OXYGEN, NAKOSA HEWA" |
Monday, July 5, 2010
UMESIKIA HII YA MCHUNGAJI?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kama hii ni kweli basi ni tanzia. Ingekuwa kwenye hizi nchi za wenzetu huyu Mchungaji angeburuzwa kortini au angelipishwa mamilioni ya dola!
ReplyDeleteKatika maisha yetu haya yanayokwenda kasi, mambo madogo (japo ya muhimu sana) tunayapiga kumbo. Kuna funzo kubwa hapa!
Kweli kaka kama kwa jamaa zetu bonge la fidia
ReplyDelete