Monday, June 21, 2010

IFAHAMU RADIO

Redio ni chombo (kifaa) kinachopokea mawasiliano kutoka katika kituo cha redio na kuyabadilisha kuwa sauti.
Kwa kawaida redio inapokea kwa njia ya antena yake mawimbi sumakuumeme yanayosambazwa na antena ya kituo cha redio. Pia kuna aina za redio ambazo mawasiliano hufika kwa umbo la alama za umeme katika waya. Mawasiliano ya sumakuumeme yanasambazwa pia kwa njia ya chomboanga au satelaiti lakini njia hii inahitaji vyombo maalumu na antena ya kawaida haitoshi.
Mwaka 1886 Mjerumani Heinrich Hertz alitambua mawimbi ya sumakuumeme. Wataalamu na muhandisi mbalimbali walifanya majaribio katika miaka iliyofuata kutumia mawimbi haya kwa mawasiliano, kati yao Mwitalia Guglielmo Marconi, Mwamerika Nikola Tesla na Mrusi Alexander Popov. Kila mmoja ametajwa kama "mtu wa kwanza áliyegundua redio".
Kituo cha kwanza cha redio kilianzishwa na Mholanzi Hanso Schotanus à Steringa Idzerda tar. 6 Novemba 1919 aliposambaza muziki kutoka nyumba yake. Kituo cha kwanza cha kibiashara kilianza kazi mwaka 1920 Marekani mjini Pittsburgh.
Katika miaka iliyofuata redio ilisambaa kote duniani. Ni njia muhimu ya kusambaza habari pamoja na utamaduni hasa muziki.

No comments:

Post a Comment