Tuesday, August 3, 2010

CHURA NA MAISHA YAKE

Maisha ya chura yanaanza kama yai lililotegwa kwenye maji pamoja na mayai maelfu. Chura anatoka kwa umbo la ndubwi (pia: kiluwiluwi) ambayo ni funzo ya chura anaendelea na kipindi cha kwanza cha maisha yake katika maji. Anapumua kwa yavuyavu na mwanzoni hana miguu bali mapezi kama samaki na mkia. Viluwiluwi wengi wakiwa kwenye maji wanakula majani au mwani hata  baadaye kama chura mzima wanakula wanyama wengine.
Baada ya muda kiluwiluwi anakuza miguu minne na mapafu. Utumbo unabadilika na kujiandaa kwa chakula kipya kinachopatikana kwenye nchi kavu. Umbo linaelekea kufanana zaidi na zaidi chura mzima.
Kipindi hiki cha utoto kwenye maji kinadumu kati ya wiki tatu hadi miaka miwili kutegemeana na spishi za chura. Mara nyingi ni kama wiki 10 - 15.

No comments:

Post a Comment