Tuesday, August 31, 2010

HATIMAYE MWENYE POCHI AMEPATIKANA

Habari njema ni kwamba yule tuliyekuwa tunamtafuta baada ya kupotelewa na pochi yake amepatikana. Dada Esther Ibrahim Shedafa aliyepotelewa na pochi hiyo iliyokuwa na nyaraka muhimu alipoatikana usiku wa jana tarehe 30 Agost 2010 na ameshakabidhiwa nyaraka zake zilizookotwa tarehe 29 Agost 2010.

Baada ya kupata nyaraka zake alishuruku sana kwa hilo na pia aliiambia blog hii kuwa nyaraka zake zote muhimu amezikuta salama.

Nasisi tunasema tunapenda kutoa shukurani kwa blog hii kutoa habari hiyo, blog ya Shein Rangers Club(http://www.sheinrangers.blogspot.com/) na blog ya jamii ya Isaa Michuzi (http://www.issamichuzi.blogspot.com/) pia tunapenda kutoa shukurani kwa watanzania wote waliotoa maoni yao kupitia blog zote hizo na katika Facebook.

No comments:

Post a Comment