Sunday, August 1, 2010

JAMAA APANDA KIZIMBANI KWA KUNAJISI KONDOO

Jamaa mmoja mkazi wa Morogoro aliyetambulika kwa jina la Gelvas Peter amepandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Mvomero mkoani humo kujibu tuhuma za kumnajisi mnyama (kondoo). Inadaiwa Bw Gelvas akijua kuwa anatenda kosa alimvizia kondoo aliyekuwa amefungwa kamba na kumfanyia kitendo hicho cha kinyama, baada ya kufikishwa mahakamani mtuhumiwa alikana shitaka linalomkabili katika kesi hiyo iliyovuta hisia za wakazi wengi wa mji huo. Kesi imeahirishwa hadi tarehe 11 Agost 2010.

2 comments:

  1. ama kweli huu ni unyama mkubwa kabisa. Huu sasa ni mwisho wa dunia!!

    ReplyDelete
  2. ni jambo la kushangaza litendwalo na binadamu

    ReplyDelete