Sunday, August 22, 2010

VUVUZELA NDANI YA KAMUSI YA OXFORD

Kamusi maarufu ya kiingereza ya Oxford imeliingiza jina la Vuvuzela katika kamusi yake ya kiingereza na kuanza kutumika katika lugha hiyo. Vuvuzela ni kati ya maneno 2,000 mapya ambayo yameingizwa katika kamusi hiyo. Vuvuzela ni tarumbeta la plastiki na lilipata umaarufu sana duniani wakati wa fainali za soka za kombe la dunia zilizofanyika nchini Afrika Kusini mwaka huu.

No comments:

Post a Comment