Tuesday, August 24, 2010

WASHITAKIWA WAVUA NGUO MAHAKAMANI

Jamaa watatu ambao wanashitakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Morogoro kwa kesi ya mauaji, walitoa kituko cha mwaka Mahakamani baada ya kuamua kuvua nguo zote na kubaki uchi wa mnyama. Sababu kubwa ya kufanya kituko hicho ni madai yao kuwa kesi yao imechukua muda mrefu na hatma yake haifahamiki.

Watuhumiwa hao ambao ni Sijali Ally, Adamu Ramadhani na Msafiri Abdallah wanakabiliwa na shtaka la mauaji ya mlinzi wa Hoteli moja mkoani Morogoro. Jamaa hao walifanya kituko hicho mbele ya Hakimu Mkazi Nuru Nassary baada ya kusikia jalada la kesi yao bado halijarudishwa toka kwa mwanasheria mkuu wa Serikali na kesi yao imeahirishwa.

No comments:

Post a Comment