Friday, September 24, 2010

IJUE POMBE NA MADHARA YAKE

Pombe ni aina ya kilevi ambayo ipo kwa mfumo wa maji na ndani yake kuna dawa inayoitwa Alcohol. Dawa hiyo ya Alcohol utokana  sukari au vitu vyenye asili ya sukari vikishachacha/haribika.

Madhara ya pombe:
Alcohol iliyopo ndani ya pombe udhuru sehemu mbalimbali katika mwili wa binadamu, madhara huwa makubwa na mabaya zaidi iwapo pombe itanywewa mara kwa mara, na hasa utumiaji wa  pombe kali. Sehemu zifuatazo ndizo upata madhara zaidi katika utumiaji wa pombe.
Ini - hii uharibika vibaya na kuwa kama kitu kilichoungua kwa moto.
Tumbo - Alcohol uweza kuchubua ngozi laini ya tumbo la chakula na kusababisha vidonda vya tumbo.
Ubongo - Baadhi ya chembechembe za ubongo (brain cells) huaribika na kusababisha kupunguza kumbukumbu.
Mimba- Unywaji wa pombe usababisha kuharibika kwa mimba, pamoja na kusababisha kuzaliwa kwa mtoto asiyekuwa na akili timamu (mtindio wa ubongo). Pia pombe uweza kuleta madhara katika moyo na mapafu ya binadamu.

No comments:

Post a Comment