Monday, September 13, 2010

JAMAA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUISHI NA KIMADA MTOTO WA MIAKA TISA

Jamaa mmoja mkazi wa Mikese mkoani Morogoro, Bwana Omary Mrisho ametoa kali ya mwaka baada ya kubainika anaishi na kimada mtoto wa miaka tisa (9). Na sasa jamaa huyo ameshapandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro.

Inadaiwa mtuhumiwa huyo alikuwa akiishi na mtoto huyo tangu Desemba mwaka jana na alikuwa hasomi, inasemekana jamaa alikuwa anaishi na mtoto huyo akimfaya kimada wake na alikuwa akifanya nae tendo la ndoa kwa kumpaka mafuta.

Jamaa huyo aliyefanya unyama huo amefikishwa Mahakamani kwa kosa la kubaka, hukumu ya kosa la kubaka ni miaka siyopungua thelathini jela.

4 comments:

  1. Je mtu kama huyu atapewa adhabu gani ili iwe fundisho, sidhani katika karne hii mtoto wa miaka tisa anaweza kuvunja ungo? huu ni unyama na kama sheria haitachukua mkonod wake ipo siku wananchi wataamua la kuamua!

    ReplyDelete
  2. Mie naona kuna haja ya kuangalia upya sheria kwa watu wanyama kama hawa!

    ReplyDelete
  3. Huyo jamaa hana hata hadhi ya kuitwa nusu binadamu

    ReplyDelete
  4. chib...... dalili za dunia kufika ukingoni hizi sasa!!

    ReplyDelete