Sunday, September 19, 2010

JAMAA MLEVI ATEMBEA NA RISASI KICHWANI BILA KUJIJUA

Jamaa mmoja mwenye sifa ya ulevi nchini Ujerumani amegundulika ana risasi kichwani kwake baada ya kukaa nayo kwa miaka mitano bila kufahamu. Inasemekana jamaa huyo mwenye asili ya Poland na mkazi wa jiji la Berlin nchini humo alipigwa risasi akiwa amelewa chakali.

Jamaa huyo anadai siku moja akiwa anapata kiraji alikumbana na mkasa wa kupigwa na kitu kichwani kwake lakini akadharau na kuendelea kupiga maji  (pombe).

Haya hivyo, alikuwa akisumbuliwa na maumivu makali ya kichwa mara kwa mara hadi alipoamua kwenda hospitali kwa uchunguzi zaidi. Na ndipo jopo la madaktari bingwa walipogundua kuna risasi ya ukubwa wa 5.6mm kichwani kwake.

Ushauri wa bure: kwa wapiga kiraji kuwa wasidharau  hali yoyote ambayo si ya kawaida endapo itajitokeza wakati ukiwa unakata maji. Ili kuepuka kutokewa na mambo kama hayo ya kukaa na risasi kichwani kwa miaka mitano bila ya kujitambua, kisa pombe.

No comments:

Post a Comment