Thursday, September 16, 2010

JIJI LA NAIROBI NA VITUKO VYAKE

Jiji la Nairobi ni moja ya majiji makubwa barani Afrika, jiji hili kubwa na maarufu katika ukanda wa Afrika mashariki na kati huwa halikaukiwi vituko kama yalivyo majiji mengine makubwa duniani. Kituko cha aina yake kimetokea katika mitaa ya  Hulingham ndani ya jiji  hilo baada ya Polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna jamaa wawili wanafanya biashara haramu ya kuuza viungo vya binadamu.

Polisi hao waliweka mtengo na kufanikiwa kuwakamata jamaa wawili mmoja ni mfanyabiashara na mungine ni mfanyakazi wa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Kenyata, baada ya kupekuliwa kweli walikutwa na viungo vya binadamu katika mfuko wa plastiki. Viungo walivyokutwa navyo ni sehemu za siri za  mwanaume. 

Jamaa hao walikamatwa na upelelezi ukikamilika watafikishwa Mahakamani.

2 comments:

  1. Jamani watu wa haki za binadamu mpo wapi, au haki hizoo ni wakti mtu akiwa mzima? Manake hebu jiulizeni, huyu anakatwa viungo vyake bila ridhaa yake, nani atamtetea, au kwa vile ni maiti hana thamani, najiuliza na kukosa jibu!

    ReplyDelete
  2. Mkuu ukifatilia unakuta jamaa wanauza kwa watu wenye imani za kishirikina!

    ReplyDelete