Thursday, September 30, 2010

JE UNAJUA HILI LA WAAMUZI WATOTO

Waamuzi wa mpira wa minguu watoto chini ya miaka 14 walichezesha mchezo wa majaribo kati ya timu ya Taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) na  timu ya kituo cha soka cha Twalipo katika uwanja wa karume.na kuumudu mchezo huo. Waamuzi hao watoto (pichani juu wenye  jezi za njano) ambao wanalelewa na kituo cha soka cha Twalipo ambacho kipo chini ya Jeshi la Wananchi Tanzania walichezesha mchezo huo kwa umahili mkubwa na kumwagiwa sifa kem kem na wadau wa mchezo huo.

Iwapo taasisi na vituo vingine vya michezo vitaiga mfumo huu wa kuwaanda watoto kuwa waamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu basi tatizo la kufungiwa kwa waamuzi na kulalamikiwa kila wakati litapungua na hatimaye kuisha kabisa. Inasemekana moja ya vikwazo katika maendeleo ya mpira wa miguu nchini ni ubovu wa  waamuzi wa mchezo huo ambao  unapendwa na mamilioni  ya watanzania.

No comments:

Post a Comment