Thursday, September 2, 2010

KISA CHA MIMI NA DAKU

Miaka mingi kiasi iliyopita mwezi kama huu nakumbuka niliwahi kutoa kituko cha mwaka, naweza kusema inaweza ikawa sio kituko ila ni kutokuelewa kitu nilichokuwa nakisikia kila siku ifikapo mwezi kama huu yaani mwezi wa mfungo wa Ramadhani.

Ilikuwa kila panapofika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani nilikuwa nasikia watu pale nyumbani wakizungumzia kula daku na mie kila siku nilikuwa nataka kujua hicho chakula yaani daku aina gani ya chakula. Basi kila niliyekuwa namuuliza alikuwa ananijibu nitakuamsha uone lakini matokeo yake wananisahau kila siku na mie nikiamka asubuhi nakuwa mkali kwa kutoamshwa kula hicho chakula kiitwacho daku.

Hatimaye siku ya siku ikawadia nakumbuka alikuja kuniamsha kaka yangu mmoja mkubwa ilikuwa kama hivi:-
Kaka: we hamka ukale daku
Na mie kweli nikaamka hadi mezani kwa ajili ya kula daku
Mimi: Haa kumbe daku yenyewe wali na maharage sitaki narudi kulala
Jamaa walicheka sana, na mie nilishangaa kukuta wali na maharage, mie nilikuwa najua daku ni aina ya chakula tena kitakuwa kizuri sana maana watu wanaamka kula usiku?

Hii ni kweli tupu!!


No comments:

Post a Comment