Saturday, October 2, 2010

ABRAMOVICH ASHIKA NAMBA 50 KWA UTAJILI DUNIANI

Roman Abramovich ambaye anamiliki kampuni ya Mill House LLC inayojihusisha na biashara ya mafuta, anahesabiwa kuwa ana utajiri wa dola bilioni 11.2 kwa mujibu wa jarida la Forbes la nchini Marekani.
Kiutajili duniania anashika nafasi ya 50 na kwa nchini kwake Russia (Urusi) anashika nafasi ya nne.

Abramovich alizaliwa mwaka 1966 na wazazi wake ni mchanganyiko watu wa Russia na Israel na mwaka 2003 aliteuliwa kuwa mfanyabiashara bora wa mwaka nchini Russia.

Pamoja na umaarufu wake na utajili mkubwa lakini alianza kujulikana diniani baada ya uamuzi wake wa kununua timu ya mpira wa miguu ya Chelsea mwaka 2003 ambayo anaimiliki mpaka hivi sasa. Pamoja na Chelsea pia anazisaidia timu za CSKA Moscow na timu ya taifa ya soka ya Russia.

Kutokana na utajili wakea Abramovich ana walinzi 40 na inasemekana ndio mfanyabiashara mwenye walinzi wengi zaidi duniani.

No comments:

Post a Comment