Tuesday, October 5, 2010

BENDERA YA UFILIPINO YAPEPERUSHWA KIMAKOSA MAREKANI

Serikali ya Marekani imeomba msamaha kwa serikali ya Ufilipino, baada ya kufanya kosa la kugeuza bendera ya nchi hiyo juu chini. Tukio hili lilitokea jijini New York nchini Marekani wakati Rais Obama alikuwa akikutana na Rais Benigno Aquino wa Ufilipino.

Msemaji wa ubalozi wa Marekani nchini Ufilipino, Rebecca Thompson amekili kutokea kwa kosa hilo na kusema ni kosa kubwa na la kibinadamu linapaswa kusamehewa. Bendera hiyo yenye rangi nyekundu, nyeupe na bluu yenye nyota za njano iligeuzwa huku rangi nyekundu ikiwa juu badala ya kuwa chini.

Bendera ya Ufilipino inapogeuzwa inahashiria nchi hiyo imeingia katika vita.

2 comments:

  1. Wenzetu wapo makini na wanaomba radhi...je ingekuwa huku kwetu Africa...unajua ...eeeh, omba radhi kwanza, na kukubali makosa, ikibidi unaachia ngazi kuonyesha ukomavu!

    ReplyDelete
  2. Hili ndio somo tosha kwa nchi zetu za kiafrika na wale wote wasiotambua makosa yao na kuomba radhi.

    ReplyDelete