Monday, October 18, 2010

IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA ZAINGIA UCHAGUZI MKUU

Imani potofu za kishirikiza zimeingia katika vichwa vya wananchi wakati huu taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu. Imana hizi sasa zinagusa watu katika kampeni zao za kunadi sera na wagombea wao, hivi karibuni inadaiwa kuwa kuna kundi la waganga wa kienyeji limeingia kisiwani Pemba kwa lengo la kuroga uchaguzi.

Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa CUF jimbo la Wawi, wilaya ya Chakechake mkoa wa Kaskazini Pemba katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja shule ya sekondari ya Fidel Castor alipokuwa akimnadi mgombea ubunge wa chama hicho Hamad Rashid Mohamed.

Mwenyekiti huyo aliongeza kwa kusema kundi hilo la waganga limeingia kisiwani Pemba likiwa na mbuzi kwa lengo la kuroga uchaguzi pia alisema dawa pekee ya kupambana na waganga hao wenye nia ya kuharibu uchaguzi ni kufunga kwa siku tatu kabla ya uchaguzi.

Kwa hili kuna umuhimu wa kutolewa elimu kuhusiana na uchaguzi mkuu ili imani hizi zisichukue nafasi katika kipindi hiki cha kampeni, wakati wa uchaguzi, wakati wa kuhesabu kura na wakati wa kutangaza matokeo vituoni. Kufumbiwa macho kwa imani kama hizi kunaweza kuhatarisha amani na utulivu uliopo nchini kwa sasa.

No comments:

Post a Comment