Friday, October 15, 2010

MAGAR AMPIKU NINO KWA UFUPI DUNIANI

Khagendra Thapa Magar mwenye umri wa miaka 18 wa Nepal ambaye ana umbile la mtoto mdogo ameingia katika rekodi ya  kuwa mtu mfupi zaidi kuliko wote duniani zinazoandaliwa na  kampuni ya Guinness ya nchini Uingereza inayoweka rekodi  za matukia mbalimbali ya ajabu duniani.

Magar ambaye ana urefu wa inchi 26.4 sawa na sentimita 67, ametunukiwa cheti cha kuwa mtu mfupi kuliko wote duniani baada ya kumshinda Edward Nino Hernandez wa Colombia ambaye ana urefu wa inchi 27 ikiwa sawa na sentimita 70. Nino alikuwa akishikilia rekodi ya kuwa mtu mfupi kuliko wote duniani.

Kwa mujibu wa daktari anayemuhudumia Magar kwa muda wa miaka mitano iliyopita anasema Magar ana umbo la mtoto wa miaka mitatu pia uwezo wake wa kufikiri na tabia zake ni za mtoto mdogo.

No comments:

Post a Comment