Friday, October 22, 2010

WAKATAA TRENI WAKIDAI NI MASHETANI

Wakazi nchini Croatia wametoa kali ya mwaka kwa kutoa madai mazito kwa serikali ya nchi hiyo kwa kuitaka kuchukua hatua za haraka kufuta huduma ya usafiri wa treni nchini humo.

Sababu kubwa ya wakazi hao kutoa madai hayo ni vifo vya maelfu ya watu kutokana ajali zitokeazo kila mwaka na kuhusisha huduma hiyo ya usafiri na imani za kishirikina na kudai kuwa ndani ya vyombo hivyo vya usafiri kuna mashetani ambayo yamekuwa na tabia ya kunyonya damu za watu. Inasemekana ajali za treni zimesababisha vifo vya watu 954 ndani ya mwaka nchini humo.

No comments:

Post a Comment