Friday, October 22, 2010

TAJ MAHAL JENGO ZURI LENYE KABURI


Taj Mahal (Kiajemi taji la mahali) ni jengo zuri la kaburi lenye umbo la msikiti mjini Agra (Uhindi). Mara nyingi huhesabiwa kati ya majengo mazuri duniani.
Taj Mahal ilijengwa 1631 - 1648 kwa amri ya Shah Jahan aliyekuwa mtawala wa nasaba ya Moghul aliyetaka kumkumbuka mke wake mpendwa  Mumtaz Mahal. Shah Jahan aliwa ajiri mafundi 20,000 kutoka Asia ya Kusini na Asia ya Kati walioongozwa na Mwajemi Ali Fazal kutoka Afghanistan. Msanifu huyu aliunganisha sifa za ujenzi wa Uajemi na Uhindi.
Taj Mahal imekuwa shabaha ya watalii wengi na tangu 1983 imeandikishwa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO.
Jengo liko hatarini kutokana na hewa chafu. Magari hayaruhusiwi kukaribia jengo katika duara ya kilomita 2. Hata hivyo gesi chafu na mvua asidi zinaendelea kula mawe yake.

2 comments: